GET /api/v0.1/hansard/entries/1104462/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1104462,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1104462/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Marwa Kitayama",
    "speaker": {
        "id": 13394,
        "legal_name": "Marwa Kemero Maisori Kitayama",
        "slug": "marwa-kemero-maisori-kitayama"
    },
    "content": "unaendeleza maisha yetu na afya zetu, lakini pia vipengele vyake visije vikawa kwamba vinazuia tusifikie tiba kwa yule mtu ambaye hana uwezo ama madaktari hawako kwa karibu kuweza kupata kile tunaita prescription. Pili, Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni vizuri tukubali kwamba chakula na dawa vinaingiliana. Mswada huu unalenga kwamba tuweze kudhibiti mambo haya kwa pamoja. Ni kweli. Lakini, unaweza ukaona kwamba tendo la kula chakula kizuri lenyewe ni tiba. Vile vile, kupata dawa nzuri yenyewe ni tiba. Ndio maana nasema ni vizuri tusitofautishe mambo haya. Yanaelekea vizuri. Yanapendeza, ndio. Lakini, ingependeza zaidi kama tungeangalia mambo ya dawa yaende katika laini yake na yale ambayo ni ya chakula yaende katika laini yake. Ndiyo maana napendekeza kuwe na marekebisho ya kutofautisha ili mambo ya dawa yaangaliwe kivingine na haya ambayo ni ya chakula yaangaliwe kivingine. Mwisho, sheria nzuri ni ile ambayo inafanya kazi kwa urahisi na inaeleweka vile vile kwa urahisi, ili yule mama ambaye yuko pale nyumbani asije akapatikana katika ile hali ya kunyanyaswa kwa sababu sheria ni ngumu kwake kuelewa. Ndio maana kutofautisha kutarahisisha kidogo kwa sababu tuna taratibu zetu za tangu jadi ambazo tunaishi nazo. Yule mama ambaye yuko pale kijijini atajua jambo hili liko hivyo kwa sababu ni kawaida. Lakini tukiingiza katika usomi huu halafu tukamshurutisha kwamba afuate hayo na kwamba kuna sheria ilihali yeye anajua akiondoka atachuna matawi fulani akaweze kupata tiba, itakuwa pia tunamzuia na kumushurutisha kwamba akaishi maisha yake kwa kuwa na wasiwasi kwamba huenda alichokuwa akifanya na ni kizuri kinakuwa tatizo. Kwa hivyo, ninasapoti Mswada huu sana lakini nasema kwamba ingependeza zaidi kama tungetofautisha ili tuwe na kile kinaangalia mambo ya dawa na iwe ilivyo na kile kinaangalia mambo ya lishe na chakula kiwe tofauti. Hii ni kama walivyofanya nchi zingine ili tusiwe tunatengeneza sheria ambayo baada ya miaka miwili tutagundua kwamba haifai na tunarudia tena. Kwa mfano, walivyosema wenzangu, kama Marekani walianza mwaka 1920 na wao wakagundua kwamba inabidi watofautishe, mbona sisi tusianze moja kwa moja kwa kuchukua kile Wazungu wanaita best practice na kuanza hapo na hapo na kuendeleza kwa haraka haraka? Kwa hivyo, katika ile Kamati ya Nyumba Nzima au Third Reading, nitapendekeza tuwe na huo utofauti lakini in principle, uhai wa Mswada huu upo. Mswada huu ni mzuri. Ni Mswada unaoendeleza afya zetu. Vile vile, unawachunga Wakenya wasihangaishwe na watapeli ambao tumewaona hapo nyuma kidogo tulipokuwa tukisafiri katika mabasi haya ya umma. Ungekuta kwamba anaingia mama ama anaingia baba na anaanza kuuza madawa kwenye mabasi hayo na hakuna udhibiti wa aina yoyote ile. Kwa hivyo, ninaamini huu ni Mswada mzuri na utatusaidia ili tuweze kufikia mahali pa kutofautisha haya mambo mawili moja kwa moja kabla ya kuenda mbele halafu baadaye kuwe na haja ya kufanya hivyo. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono marekebisho hayo."
}