GET /api/v0.1/hansard/entries/1104802/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1104802,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1104802/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gona",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante kwa kukubaliana na mimi. Kweli bei ya vitu vimepanda na kama mna ufahamu huo nashukuru. Hawa mabwana tunawazungumzia hapa, wao mafuta hununuliwa hata hawajui inauzwa bei gani. Sisi ndio tunapiga kelele tunasema mafuta imepanda lakini wao hawajui. Hivi ving’ora sisi Wabunge ambao tunawakilisha wananchi haturuhusiwi kwenda na kusindikizwa na askari. Lakini huyu ambaye hakuchaguliwa anakibendera akipeperusha. Anapeperushia nani bendera hii barabarani na hana jukumu lolote na mwananchi. Mamlaka yote wamepewa wao. Juzi tumeenda Mombasa na Kamati ya Barabara na Ujenzi. Tukifika kule tumesubiri Waziri na ujue tumetumia pesa za Serikali kutufikisha sisi kule. Tumefika, hakutuma mtu yeyote na hakuna barua wala lolote. Yeye mwenyewe hakuja na ni mawaziri hao. Bw. Spika wa Muda, sasa sisi hatuna mamlaka ya kuwatoa makazini lakini Bunge la Kitaifa liko na mamlaka hayo. Jamani kama umemuoa mwanamke na hazai, wakati wa kuzaa unang’ang’ana na anazaa mtoto wa kufa maanake hataki kusikia uchungu. Maanake uchungu wa kuzaa ukiambiwa usukume ama “push” kwa Kiingereza, hiyo kusukuma sio rahisi. Hasa kuna wengine huwa waoga kusukuma hawasukumi. Wanangoja mtoto akufe ndio azaliwe. Sasa hana faida mwanamke huyo."
}