GET /api/v0.1/hansard/entries/1105260/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1105260,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1105260/?format=api",
    "text_counter": 438,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, nashukuru Mhe. Sankok kwa kuleta hii habari ya Laikipia katika hili Jumba. Hata ninapomshukuru, mambo ya Laikipia siyo ya leo wala jana. Mambo ya Laikipia yamekuwepo. Vita vimekuwepo. Mazungumzo ya Jumba hili hayatatatua shida hiyo. Kile kitatatua jambo hili ni watu kukaa chini na kujua shida ya Laikipia kwa sababu unaweza kufikiria ni jamii mbili tu ndizo zinasikia uchungu; Pokot na Samburu. Hii ni kwa sababu gani? Kila kabila la Kenya liko Laikipia, lakini shida ambayo iko Laikipia ni shida ya kawaida. Kila mara ikiwa imebaki mwaka moja kabla ya uchaguzi, lazima shida itokee Laikipia na watu kuumia; wenye hatia na wale ambao hawana hatia. Hii ni kwa sababu ya nyasi. Tunaambiwa kuwa nyasi ndiyo inaleta shida. Watu huwa wanaenda kutafuta nyasi Laikipia. Kuna watu wamenunua mashamba huko. Hakuna Mkenya ambaye hajanunua shamba Laikipia. Hata Wasamburu wengi wamenunua shamba Laikipia. Lakini ile shida iko na ile inatushangaza kabisa ni kuwa ng’ombe wanauliwa na ni wanyama ambao hawaongei. Wale ambao wanachunga ng’ombe ndio wanafaa kufungwa kama wamewaingiza kwa mashamba ya watu ili wale nyasi. Hii ni bora kuliko kuua ng’ombe kwa kuwapiga risasi na hali hawana hatia. Hiyo ni kumaliza mwenye anategemea hao ng’ombe. Ninavyoongea sasa hivi, kuna mzee mmoja ameishi Laikipia kwa miaka 35 na ng’ombe wake, karibu 35, waliuawa juzio. Hiyo inaumiza mtu kwa sababu hana chanzo cha mapato isipokuwa hao ng’ombe. Mwaka wa 2009, Laikipia ilikuwa imeoza kabisa na tulianzisha Peace Caravan na kwa miaka 11, vita hivi havijawahi kutokea hadi juzi. Bunduki haiwezi leta amani Kenya. Ni lazima watu wakae chini na kujua shida iko wapi kwa sababu shida ya Laikipia sio juu ya nyasi tu. Hakuna mtu anafurahia mtu mwingine kuuawa ama kufukuzwa kwa shamba lake. Hakuna mtu anafurahia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}