GET /api/v0.1/hansard/entries/1105261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1105261,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1105261/?format=api",
    "text_counter": 439,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "hilo. Hakuna mtu pia anayefurahia ng’ombe ambao ni mali ya mtu kuuawa na abaki bila chochote. Hakuna mtu anafurahia kitendo hicho. Kwa hivyo, kila mtu ana shamba huko na watu wamenunua mashamba huko. Kama mtu amenunua ama amenyakua shamba ya Serikali hawezi kuenda na kusema: “Nimepeana shamba; kujeni basi mchukue ama mgawanyiwe.” Tunagawanyiwa na nani? Kwa hivyo, ikiwezekana, kama viongozi wa Laikipia, Samburu, Isiolo na Pokot, tunafaa kukaa chini sisi sote na kujua tatizo liko wapi na tulitatue, kwa mfano, kwa kukabiliana Serikali kama ndiyo inatuletea shida ya kupigana na bunduki na wakuje watuambie. Tunavyoongea hivi kama watu wa Samburu, Isiolo na Laikipia, haiwezi kusaidia. Kwa hivyo, ninahimiza viongozi wote tukae chini na tupate kujua taabu ya Serikali hadi kutumia risasi na ndege kupiga watu. Hivi sasa, vita vinavyoendelea Laikipia vinaleta shida nyingi kwa sababu…"
}