GET /api/v0.1/hansard/entries/1105807/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1105807,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1105807/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "lilijibiwa magazetini na vyombo vingi vya habari. Hiyo sio taratibu ya sheria zetu za Kenya. Swali lolote likiulizwa hapa Seneti, Mawaziri wanafaa kujibu Seneti kwa heshima. Swali likiulizwa hapa Seneti, halifai kujadiliwa mahali pengine isipokuwa hapa ndani. Seneti kupitia Sen. Olekina alitaka kujua kama Wizara husika linajua kwamba watu wengi kutoka Bara la Asia wanaingi nchini kwa kuwa jambo hilo linawezakuleta mtafaruku wa amani. Ikiwa Mawaziri watakuwa wanajibu Seneti kupitia magazeti na vyombo vingine vya habari, nimngependa kusisitiza kwamba sio haki sisi kujibiwa na Mawaziri wakiwa wameketi katika ofisi zao. Seneti ikitaka mawaziri hao waje hapa kujibu maswali, lazima waje hapa. Sio vyema kwa mawaziri hao kuipa Seneti majibu kupitia vyombo vya habari. Seneti ina sheria zake ambazo lazima ziheshimiwe. Mhe. Seneta yeyote akiuliza swali hapa, hafai kupokea jibu kupitia vyombo vya habari au kupitia Bunge la Kitaifa. Hatukubaliani na mwenendo wa Mawaziri wengine kwa sababu hiyo sio sharia au haki. Bw. Spika wa Muda, nasisitiza kwamba Seneta yeyote akiuliza swali hapa, lazima lijibiwe kwa heshima. Viongozi wote walio hapa Seneti ni watu waliobobea kielimu na katika siasa. Kwa hivyo, ni lazima Seneti iheshimiwe na Mawaziri kama wanavyoheshimu Bunge la Taifa. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}