GET /api/v0.1/hansard/entries/1106362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1106362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1106362/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta, CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": "kwa sababu wengine wana matatizo na changamoto zao. Hawajakuwa na uwezo wa kulipia vyeti ambavyo vimefanywa kuwa lazima ili waweze kupata ajira. Vijana wengi wanatoka kwa familia ambazo zina chanagamoto. Wengine wamesoma kupitia ufadhili na misaada kutoka kwa wasamaria wema. Familia kama hizo haziwezi kabisa kulipia vyeti hivyo. Watoto wengine ni mayatima. Nimekumbana na wengi sana ambao wamesoma kwa shida na wamepita mitihani vizuri. Wako na vyeti vizuri ambavyo vinaweza kuwasaidia kupata ajira. Lakini suala la kupata vyeti hivi limekuwa mojawapo ya vikwazo ambavyo vinawachuja kwenye kinyaganyiro cha kutafuta kazi. Nampongeza sana Mheshimiwa Keter kwa kuleta Mswada huu Bungeni ili tuweze kuujadili. Kama viongozi, ni lazima tuithibiti hali hii na tuweze kusimama na vijana wetu. Ni vyema tuondoe hili suala la mtu kuwa na hivi vyeti anapotafuta ajira. Tumewaona vijana wengi wakiwa na msongamano wa mawazo. Watu wamejitia vitanzi kwa sababu wameambiwa ni lazima wawe na hivi vyeti na wameshindwa kuvipata, na wakapatwa na msongamano wa mawazo na wakajiuwa. Gharama ya maisha nchini Kenya imepanda. Bei ya mafuta imepanda sana. Tusipoweza kuithibiti hali kama hii tutapata kesho tukiambiwa kuwa hata wale akina mama mboga sokoni watawekewa masharti ya kuwa na vyeti fulani ndiyo wao pia waweze kufanya biashara zao. Kwa hivyo, ni vyema kuwa Mswada huu umefika Bungeni. Ninaunga asilimia mia ili vijana wetu waweze kupata afueni na wajisikie wako huru ili waweze kutafuta kazi bila vikwazo wanapomaliza masomo yao. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}