GET /api/v0.1/hansard/entries/1106394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1106394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1106394/?format=api",
    "text_counter": 21,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika. Ninamtolea kongole ndugu yangu, Sen. Githua Ngugi kwa kuteuliwa na kuja katika Bunge la Seneti. Yeye kama Seneta mteule ako na majukumu mengi ambayo anatakikana kuyatekeleza. Mrengo wa Jubilee ulikupa nafasi hii. Wewe ni kijana na uko na maisha marefu ya kuishi ndani ya hili Bunge kulingana na uwezo au utendakazi wako. Kwa hivyo, tekeleza wajibu wako uliokuleta hapa Seneti. Kuna mambo mengi utajifunza. Hili ndilo Bunge ambalo linajulikana Kenya nzima. Liko na wasomi kama wewe. Kwa hivyo, tuonyeshe ujasiri na elimu yako kulingana na vile utatendakazi hapa ndani ya Bunge la Seneti. Hivi sasa, ninaongea kwa Kiswahili ambayo ni lugha ya kitaifa. Unaweza pia kuongea Kizungu ambayo ni lugha ya Kitaifa. Lakini, huwezi kuchanganya lugha hizi mbili pamoja. Kwa hivyo, utachagua ni lugha gani utatumia. Zaidi ni kwamba utajifunza. Tunaye Kiongozi wa Waliowengi, ndugu yangu, Sen. Poghisio, ambaye ako na elimu ya kutosha. Taaluma yake iko juu sana. Maseneta wote wako na taaluma ya hali ya juu. Utajifunza na kujua mambo mengi yanayoendelea ndani ya Seneti. Ningependa kukupa maoni yangu kuhusu wale waliotarajia uwaangalie. Kuna ile kabila ndogo ya Ogiek ambayo ilikuwa imeomba kiti hiki. Ninakusihi na kukuomba uwafikie na kuwatumikia kadri inavyowezekana."
}