GET /api/v0.1/hansard/entries/110718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110718,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110718/?format=api",
"text_counter": 408,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Ni maombi yangu kwamba wale wachache ambao kawaida hawawezi wakapata uongozi wa nchi hii--- Nazungumzia kabila kama Mkuria, Mtaita na Mteso. Itakuwa ni vigumu sana katika Katiba hii tunayopendekeza awe rais wa Kenya. Lakini ikiwa kwamba tutaenda katika ngazi tatu, basi katika wilaya yangu najua nitasimamia rasilimali yangu. Katika mkoa wangu, nitaweka gavana wa kuangalia masilahi yangu. Tukifanya hivyo, mambo ya ukabila tutafuta katika Kenya hii na yale mengine yatakuwa yanaweza kushawishika bila kuzusha utata na umwagikaji wa damu."
}