GET /api/v0.1/hansard/entries/110719/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110719,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110719/?format=api",
"text_counter": 409,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, la mwisho ambalo nataka nizungumzie ni kwamba katika Katiba hii, kuna utata mdogo pale na pale kama vile ndugu zetu Waislamu wanavyochukulia Kadhisâ court. Zimekuweko tangu wakati wa Uhuru na nimezaliwa Mombasa na nimeishi na Waisilamu na nina marafiki zangu Waisilamu. Haijawahi kunihusu kwamba wana korti na sheria zao. Leo hii kwa nini twataka tulete utata na wana Kenya wale wachache? Maanake tukiangalia Wakristo, tuko wengi na Waislamu ni wachache. Mbona twataka tuingilie kile kitu ambacho hakituhusu sisi? Waswahili husema: âPilipili usio ila yakuwashia nini?â"
}