GET /api/v0.1/hansard/entries/110720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110720,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110720/?format=api",
    "text_counter": 410,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Mambo yale mengine ambayo tunataka tuyalete kugawanya wananchi wa Kenya ni misingi ya kusema kwamba: “oh, mimi najua maisha ya binadamu huanzia wapi!” Kila mtu ana dini yake! Mtu wa dini nyingine atakwambia kabla hajazaliwa kulingana na dini yake, ilikuwa inajulikana atazaliwa. Wengine wanajua ukidunga mimba ndio maana unazaliwa. Kwa nini tusiondoe kipengele cha kuwezesha watu kutoa mimba ili watu wote waone masilahi yao yanashughulikiwa na Bunge la Kumi ili tupate Katiba mpya? Tukisema kila mtu anakita; anasema huyu si sawa, mimi ni sawa, tutafika wakati pia tukose nafasi ya Bunge la Kumi kutoa Katiba. Naonelea, sitapoteza wakati mrefu. Tukiangalia vile nimesema, tufanye ugatuzi na tuchukulie maanani ya wale wachache. Kama ni Waisilamu, tuwape haki yao na kama ni Wakristo wale wengine tuondoee vipengele hivyo ili jina langu kama Mbunge wa Voi liingie katika historia miaka 50 ijayo kama siko katika dunia hii, jina langu pia la Mr. Dan Mwazo liwe pale kama Mbunge ambaye aliwezesha nchi ya Kenya kupata Katiba mpya. Nawaomba ndugu zangu tuunge mkono na marekebisho machache ili Katiba hii tuipatie wana Kenya na wana Kenya wawe na Katiba na sheria mpya ya kujitawala."
}