GET /api/v0.1/hansard/entries/1108219/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1108219,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1108219/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu wa Ushirikiano Baina ya Taasisi za Umma na Waekezaji wa Kibinafsi Katika Miradi ya Maendeleo. Mswada huu umekuja wakati mwafaka kabisa kwa sababu ijapokuwa Serikali imepanga kufanya miradi mingi ya kimaendeleo, miradi mingi imekwema kwa sababu ya ukosefu wa fedha za kutosha. Mswada huu utakapopita utasaidia pakubwa miradi ya maendeleo nchini kwa sababu pesa nyingi ambazo zinahitajika kutekeleza miradi zitapatikana kupitia kwa waekezaji wa kibinafsi. Mpango huu utasaidia kupatikana kwa pesa nyingi ambazo zitatumika kutekeleza miradi na huduma nyingine nchini. Bi. Naibu Spika, tumeona kwamba tayari kuna miradi inayotekelezwa katika Jamuhuri yetu ya Kenya, kwa mfano, Nairobi Express Highway. Huu ni mradi wa kibinafsi ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na Serikali yetu. Pia kuna barabara inayojengwa kutoka Westlands hadi Mau Summit. Huu ni mradi unaofadhiliwa na watu binafsi kwa kushirikiana na Serikali yetu. Mpango kama huu sio wa kwanza nchini lakini hatukuwa na sheria ya kusimamia miradi kama hii. Kila sehemu nchini inahitaji miradi, kwa mfano, barabara, nguvu za umeme na kadhalika. Hii ni miradi ambayo inasaidia pakubwa kuleta maendeleo mashinani. Ushuru au kodi tunazolipa haziwezi kujenga barabara na kutekeleza maendeleo mengi nchini. Kupitishwa kwa Mswada huu kutasaidia pakubwa kuendeleza maendeleo katika sehemu nyingi za nchi yetu ambayo sisi kama raia tutayalipia. Mswada huu unatoa nafasi kwa serikali za Kaunti kutekeleza miradi ya uwekezaji baina yake na wananchi wake. Jambo hili litasaidia pakubwa kuleta maendeleo mashinani. Kaunti nyingi zina miradi mizuri ya maendeleo, lakini ruzuku zinazotoka kwa Serikali Kuu na kodi wanazookota katika maeneo yao hazitoshi kufadhili ama kusimamia miradi wanaotaka kufanya."
}