GET /api/v0.1/hansard/entries/1108221/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1108221,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1108221/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kuna miradi ya nyumba ambayo kupitia kwa ‘affordable housing’ huwa ni nyumba za kiasi za wananchi. Miradi kama hiyo inaweza kufanyika katika kila kaunti. Hata hivyo, pesa zinazohitajika na zile zinazotoka katika Serikali kuu na kupelekwa katika serikali za kaunti kutekeleza miradi ya kawaida hazitoshi. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa, kuna Likoni, Changamwe, Hadija na Mzizima estates ambazo zinatekelezwa na waekezaji wa kibinafsi. Jambo hili limezua utata. Kama kungekuwa sheria ya uwazi kama hii tungeweza kujua ni akina nani ambao wamefaidika na miradi hii. Ripoti ingewasilishwa katika Bunge la Kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha kuna uwazi katika kutoa zabuni za miradi hiyo. Bi. Naibu Spika, naunga mkono Mswada huu kwa sababu utasaidia pakubwa kuleta maendeleo na kuweka mwongozo; vipi tunaweza kufanya miradi ya uwekezaji wa kibinafsi kwa ushirikiano na serikali zetu. Kifungu cha 65 cha Mswada huu kinasema- “Subject to Section 363(5), each County Government intending to undertake Public Private Partnership shall obtain the approval of the respective County Assembly before undertaking the project.” Lakini tukiangalia kifungu cha 63 hakina 63(3) ambacho kimezungumziwa hapa katika Kifungu cha 65. Ninawasihi wahusika waweze kurekebisha na kuhakikisha kwamba kinaoana na Kifungu cha 65(1). Hapa wanapendekeza bodi ambayo itasimamia miradi ambayo itatekelezwa kwa ushirikiano wa kibinafsi na Serikali. Hili ni jambo nzuri kwa sababu kwa sasa hakuna mwongozo wowote unaosimamia miradi kama hii. Jukumu hili limetwikwa Wizara husika ambazo zitasimamia miradi kama hiyo. Mara nyingi inakuwa ni shida kutoa mwongozo kwa sababu ya bureaucracy au daraja kutoka kwa Waziri, Katibu wa Kudumu na maofisa wengine katika Wizara, kabla mwongozo kutolewa kuhusu utekelezaji wa mradi wowote. Ninaunga Mswada huu tuupitishe ili tupate manufaa mengi ya maendeleo katika nchi yetu. Mwisho, jambo ningependa kugusia ni lazima tuwe macho kama Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa ili miradi hii itekelezwe. Ni lazima kuwe na uchunguzi mara kwa mara; yaani oversight ili tuone kwamba mwananchi hapunjwi katika kuendesha miradi kama hii. Miradi itakayofanyika iwe ni ya kudumu na fedha zinazotumika vizuri kuyatekeleza. Miradi mingi inafanywa bila uwazi au katika hali ambayo si nzuri. Si haki barabara ambayo inajengwa kudumu kwa miaka 30, baada ya miaka mitatu inaanza kuchimbuka, kufura manundu, kuwa na mashimo na kwingine inabomoka. Hiyo yote inaonyesha kwamba katika kutekeleza mradi hakukuwa na umakinifu na uangalifu wa kutosha kuhakikisha ya kwamba vifaa vinavyotumika vinastahili. Wakati mwingine mwakandarasi hatekelezi mradi kwa ustadi wa hali ya juu na huwafanya wananchi kuona pesa zao zimepotea. Ninaunga Mswada huu tuupitishe ili tupate manufaa mengi ya maendeleo katika nchi yetu."
}