GET /api/v0.1/hansard/entries/1108337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1108337,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1108337/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nisamehe kwa sababu wakati mwingine ulimi unateleza. Niwie radhi. Mimi pia ni binadamu. Bw. Spika wa Muda, kwanza ninaunga mkono Mswada huu. Mswada huu unataka kutengeneza sheria mwafaka ambayo italeta uhusiano bora ulio katika misingi ya kisheria baina ya umma na wafanyibiashara binafsi. Waswahili husema ‘kidole kimoja hakivunji chawa.’ Hii ni kanuni kwamba Serikali au umma peke yake haiwezi kutekeleza miradi bila ushirikiano na wawekezaji wa kibinafsi."
}