GET /api/v0.1/hansard/entries/1108339/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1108339,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1108339/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kote ulimwenguni, tunaona serikali zina uhusiano na wawekezaji wa kibinafsi. Ni lazima Serikali ya Kenya izingatie sheria za kisasa kama hizi ambazo zitaleta uhusiano bora baina na umma na watu binafsi. Kitu ambacho tunaona ni mfano mzuri wa kuigwa ni kwamba tukiangalia hii barabara ambayo inatengenezwa hivi sasa ya Mombasa kwenda mpaka airport, na imeunganishwa mpaka huko Kawangware, hiyo ni kumaanisha wazi ya kwamba kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa. Hizi ni juhudi ambazo lazima sisi tuzitie mkazo na tuone ya kwamba zimekita mizizi ndani ya Serikali yetu ama ndani ya nchi yetu; ya kwamba tunaweza kuleta umma na wafanyabiashara binafsi na wote wakaweza kushirikiana na maendeleo yakapatikana. La mwisho ni kwamba hata tunaona siku hizi wakati wowote ukiwa umeenda katika maeneo ya benki ama biashara kubwa, zamani tulikuwa tunakutana na wale watu ambao wamevaa nguo za kijeshi wakilinda maeneo kama haya. Lakini siku hizi, unaweza kuona kazi kama hizo zimechukuliwa na wafanyabiashara binafsi ambao wanashirikiana. Na wale askari ambao wako pale sio wafanyikazi wa pale ndani ya benki, lakini wanashirikiana na benki kuona kwamba njia mwafaka zinafuatwa na waekezaji wa pesa katika zile benki. Tumeona ya kwamba muelekeo kama huo umeweza kuleta faida kubwa katika nchi yetu na katika kuongeza biashara binafsi. Bw. Spika wa Muda, mimi naunga mkono Mswada huu ambao utatuendeleza sisi kama Wakenya. Asante sana."
}