GET /api/v0.1/hansard/entries/1108448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1108448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1108448/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza kabisa kabla ya kuchangia Mswada huu ningependa kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kuwa katika jopo la Spika la Bunge hili. Pia ningependa kukupongeza kwamba umeendesha shughuli za Bunge hili katika lugha ya kitaifa ya Kiswahili ambayo sio rahisi. Wakati mwingi imekuwa desturi ya Bunge zote za Kenya kuendesha shughuli zao katika lugha rasmi ya Kiingereza. Mswada huu ambayo uko mbele yetu wa kubinafsisha shirika la umma, umekuja kwa wakati mzuri kabisa. Miradi mingi imedorora kwa sababu kuna haja kubwa ya kupatikana nguvu-kazi ambayo ni nje ya wale ambao wanafanya kazi hiyo. Sasa tukiweka sheria mwafaka ambayo itabinafsisha itakuwa vyema. Kwa mfano, katika kaunti nyingi utaona uchafu umejaa katika sehemu za makaazi na mijini. Tukiweza kubinafsisha na kupeana mashirika mengine kufanya usafi kwa kufuata sheria hii, kazi hiyo itafanyika vizuri sana. Bw. Spika wa Muda, ukizuru hospitali nyingi katika kaunti zetu, utaona uchafu mwingi. Kwa hakika kama tunaweza kubinafsisha shughuli za usafi katika hospitali zetu, hospitali zetu zitakuwa safi. Tutapata nguvu-kazi ambayo ni nguvu mpya. Ukitembea katika mji wa Eastleigh saa hii, utaona uchafu unaotokana na takataka. Kama serikali ya kaunti ingeweza kubinafsisha shughuli ya usafi na kupeana kwa watu binafsi wasimamie usafi wa mji huo, tunawezapata mji safi. Mswada huu ni sawa kabisa. Bunge la Kitaifa limewezakupitisha Mswada huu, sisi tuungwe mkono ili tupate sheria ambayo itatusaidia sana katika miradi mbalimbali. Ikiwa tutaupitisha Mswada huu, sisi tutapata nguvu-kazi ambayo itakuwa ni kweli imebinafsishiwa shughuli na kazi katika kaunti zetu. Bw. Spika wa Muda, pia Mswada huu utaleta uwiano kati ya mashirika mbalimbali na serikali zetu za kaunti na Serikali kuu ambayo ni ya utendakazi na ile imebinafsishwa inaweza kufanya kazi pamoja. Watu ambao watakuwa nje ya Serikali ama shirika hiyo watakuwa na uwazi wa kuona kuna kazi inafanyika. Itakuwa ni watu wengi wanafanya kazi hiyo na kutakuwa na uwiano na ushirikiano wa karibu. Ninaunga mkono, Mswada huu."
}