GET /api/v0.1/hansard/entries/1109091/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1109091,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1109091/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa niweze kuwakaribisha Wabunge wa Kaunti ama MCAs kutoka Nandi. Ningetaka nikubaliane na wenzangu wengi kwamba katika Maseneta wachangamshi basi mmoja wao ni Seneta wa Nandi. Kusema ukweli, kama ingekuwa kuzungumza pekee yake ndio kunamrudisha mtu hapa Bunge, nina hakika kwamba angerudi hapa Bunge. Hata hivyo, ninaamini kuwa watu wa Nandi wanamuona na wako pamoja na yeye. Vile vile, ningependa kuwaambia MCAs wawe huru. Mnakaribishwa na pia mnaweza kufika hapa. Mimi ninayezungumza hapa, kipindi kilichopita nilikuwa MCA kule Kilifi lakini kwa njia zingine zisizoweza kuepukika nilijipata hapa. Kwa hivyo, hakuna lisilowezekana mbele ya Mungu. Kila kitu kinawezekana. Ukiwa na bidii na maoni, basi Mungu anaweza tangulia. Vile vile, katika upande wa uajiri, najua wakati huu Kaunti ziko na changamoto kubwa hasa kwa upande wa uajiri. Waajiri wengine hawalipi. Kwa hivyo, mzingatie hilo swala kwa sababu haja zetu sote kutoka Maseneta ni kuona kwamba kaunti zinafauli kwa ugatuzi. Tulifanya ugatuzi kwa sababu ilikuwa kitu cha maana kwetu sisi Wakenya. Karibuni sana. Jisikieni nyumbani. Asante."
}