GET /api/v0.1/hansard/entries/1109134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1109134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1109134/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Ninasimama kuunga mkono malalamishi yaliyoletwa kwetu kuhusu mambo ya afya na kadi za hospitali za NHIF. Kusema ukweli, watu walikufa zamani lakini hivi sasa, watu wanakufa zaidi. Wengine hawakufi kwa sababu hawangeweza kupona. Ijapo kuwa Mwenyezi Mungu ndiye huchukua roho, watu wanakufa kwa sababu wanakosa matibabu yanayohitajika kwa wakati unaofaa. Nitapeana mfano wa wagonjwa wa Korona ambalo ni janga la taifa na silo la mtu mmoja, la kujitakia wala kulileta. Lakini, ukipata ugonjwa wa Korona na ufike hospitalini na uwekwe kwa oxygen, uko na shida. Hii ni kwa sababu, ukiwekwa kwa chumba cha hali mahututi, siku mbili au tatu, utaambiwa ni laki kadhaa. Bw. Spika, unavyojua, taifa letu la Kenya kwa sasa, shida zimejaa. Mgonjwa anashindwa kupata chakula cha kila siku au cha masaa; asubuhi, mchana na jioni. Kwa hivyo, laki hizo zote atatoa wapi? Vile vile, kuna ugonjwa wa saratani. Ninasikitika sana kwa sababu mara nyingi, kina mama ndio hushikwa na ugonjwa huu. Ninavyozungumza, juzi nikitoka kaunti kuja hapa, nilienda kutembelea mgonjwa mmoja ambaye nilihusishwa niende nimuone akiwa ni mama anayetoka Eneo Bunge la Magarini, Wadi ya Garashi, kijiji cha Bate. Ni mama mdogo mwenye watoto wawili pekee. Ananyoyesha mtoto mmoja ambaye ni mdogo na hajaanza kutembea. Mama ako na saratani ya matiti na kwa hivyo, titi moja haliwezi kunyonywa. Kwa hivyo, mtoto ananyonya lile ambalo liko na saratani. Sasa, ninajiuliza kama Saratani husambaa au kurithiwa na kama mtoto ataipata. Nilifuatilia na kuambiwa hapo ilipo, inatibika lakini dosi moja inahitaji elfu 26,000. Huyu mama hajiwezi na hawezi kupata ata elfu moja."
}