GET /api/v0.1/hansard/entries/1109136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1109136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1109136/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Kwa hivyo, nikitoka hapa, nitafuata Maseneta walio hapa mnisaidie niweze kupata dosi moja alafu ning’ang’ane kupata hizo zingine. Bw. Spika, kwa hivyo, kuna haja ya kadi za hospitali zisimamie hayo magonjwa kwa sababu hatujui unavyokuja na kuingia ndani ya mwili. Mtu hujipata tu ako nao. Kama kadi itasaidia mgonjwa wa Malaria, mimi pekee yangu bila kwenda hospitali naweza ng’ang’ana na mtu akapona. Lakini, saratani ni ugonjwa ambao unahitaji watu wengi wakusanyike mahali pamoja. Taifa la Kenya lichukue jukumu la kuangalia watu wake ambao wanashikwa na yale magonjwa ambayo wanadamu hawawezi kujisimamia. Ninaunga mkono malalamishi hayo kwa dhati na nguvu zangu zote. Vile vile, ninawasihi waliomo kwenye Kamati ambayo itaangalia mambo ya afya wazingatie sana maswala haya, ili tupate majibu. Kama ujuavyo, ukiwa Mbunge, uko na taaluma zote. Kama ni daktari watakufuata kupata msaada wa daktari. Kama ni walimu, watakufuata, uwape pesa za kwenda shule. Kwa hivyo, matatizo mengi ambayo yanakumba wananchi wanakimbilia sisi viongozi. Basi tuchukue jukumu hili la kusihi Serikali ichukue majukumu yake ili tuweze kupumua kidogo tufuate mengine na Serikali ichukue mengine."
}