GET /api/v0.1/hansard/entries/1109322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1109322,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1109322/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa fursa. Ninampongeza Sen. (Dr.) Musuruve kwa kuleta Arifa hii ya Siku ya Ulimwengu ya Walimu. Kwa hakika, sisi sote tumepitia kwa mikono ya waalimu. Ualimu ni msingi mkubwa katika kutengeneza mtu awe mwanadamu kamili kwa sababu mwanadamu bila elimu hayuko kamili. Ukiangalia walimu wa Kenya wakati mwingi wanaenda kulima kwa sababu ya marupu rupu ama mshahara ile ambayo wanapata. Ukiangalia kwa kina walimu wanalipwa mshahara kidogo zaidi. Sen. Cheruiyot alisema mwalimu huwezi ukamlipa na hii ni ukweli. Hakuna pesa ambayo inaweza kumlipa mwalimu kwa sababu hata ukisema ni pesa kiasi gani bado hiyo kazi ambayo mwalimu anafanya ni mingi sana kuliko hiyo pesa. Mtoto mdogo akikaa nyumbani na wazazi wake, wanashindwa kumuelewa lakini huyo mtoto akipelekwa shule anafundishwa na mwalimu mpaka anajua jinsi ya kujitunza, kusoma na kuandika. Wakati ambapo ugonjwa wa Corona ulianza, shule zilifungwa. Wakati huo wazazi wengi walipata kizungumkuti kukaa na watoto nyumbani. Wazazi walishangaa wakasema, walimu wanaishi na hawa watoto namna gani huko shuleni? Mbali na kufundisha hawa watoto, walimu wanasaidia wazazi kulea hawa watoto. Wazazi wanachukua watoto asubuhi na kuwapeleka shuleni kisha wao wanaenda kufanya shughuli zao. Mwalimu anahangaika na hao watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni. Huyo mtoto akikaa na mzazi kwa muda mdogo, mzazi anashangaa, anasema huyu mtoto namna gani? Mbali na kufundisha, mwalimu anasaidia kulea watoto na anawalea katika maadili mazuri. Hii ndio sababu utapata kwamba watu ambao wako na taaluma tofauti, ukiwaangalia vizuri, wote wamepitia kwenye mkono wa mwalimu. Sisi tunafaa kuwashukuru waalimu na kuwapatia hongera. Wanapoenda kusherehekea siku ya Ulimwengu ya Walimu, sisi tunafaa tushirikiane nao na tuwapatie asante. Ukiwa katika Seneti hii ama Bunge la Kitaifa utampata mwalimu wako huko barabarani akitembea bado kuenda kuwafundisha watoto. Hata Rais wa Kenya alipita kwenye mikono ya walimu. Hata Rais wa Kenya amepitia katika mikono ya walimu. Na wale watu wote ambao wana magari makubwa wamepitia katika mikono ya walimu. Nina hakika kuwa Sen. (Dkt.) Musuruve pia ni mwalimu ndio maana amewakumbuka walimu. Hongera Sen. (Dkt.) Musuruve kwa kuleta Taarifa hii ambayo ni muhimu."
}