GET /api/v0.1/hansard/entries/111004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 111004,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/111004/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ili nitoe mawazo yangu machache kwa Hoja hii ya Katiba mpya ambayo iko mbele yetu. Kwanza, ningependa kusema ya kwamba tuko katika hatua zile ambazo tulikubaliana kama Wabunge na tukapitisha katika sheria ya Kenya za kutengeneza katiba yetu mpya hapa Kenya. Tulikubaliana na tukapitisha katika sheria yetu ya kwamba Kamati ya Wataalamu watafanya kazi yao. Wakimaliza kufanya kazi yao, watapeleka maoni yao kwa kamati yetu ya Bunge ya PSC. Nao, chini ya Mhe. Abdukadir walifanya kazi yao. Bunge ni hatua ya tatu. Bunge pia inahitajika kutekeleza wajibu wake. Bw. Naibu Spika wa Muda, tukitoka hapa, tutaenda kwa hatua ya nne ambayo ni wananchi wenyewe kupitia kwa kura ya maoni ikiwa wao watakubaliana na kazi yote ambayo imefanywa ama wataikataa. Wakati Bunge ilipoanza kufanya kazi yake, kulikuwa na utatanishi. Wengine wanasema kuwa tunaenda kuharibu Katiba. Wengine wanasema Wabunge wanaenda kupoteza pesa. Lakini umeona hali ambayo iko katika Bunge leo hii na jana; waheshimiwa Wabunge wanazungumza mambo bila chuki ama fitina au kukosana. Kwa hivyo, wale ambao walikuwa wanasema tusiende kuzungumza, tungewakosoa kidogo. Sisi ambao tuliamua ya kwamba tutaenda kule, kuna wengine wetu ambao pengine hawakusoma kila kipengele. Lakini baada ya hizo siku tatu, tumesoma vipengele vyote. Mhe. Abdikadir na Mhe. Namwamba walisoma kipengele kwa kipengele na ndio sababu leo hii tunazungumza kwa utaratibu. Kwa hivyo, tunataka tuongee tukijua kwamba kuna mambo ambayo lazima tupitie ikiwa tutakuwa na mazungumzo ya kisawa sawa. Bw. Naibu Spika wa Muda, nimepata nakala ya Katiba ile yetu ya zamani ambayo iko hapa. Pia, nina nakala ya Katiba Rasimu ambayo tunataka kupitisha. Kwa Kiingereza inaitwa proposed Constitution. Ukiangalia Katiba hii yetu ya zamani ambayo tumeishi nayo, ingawa imebadilishwa muda kwa muda, lakini tuko nayo mpaka sasa, ina vipengele 127. Katika vipengele hivi, Katiba Rasimu ambayo tunataka kuipitisha, ina vipengele 264. Ukiangalia mazungumzo na Hoja ya Bw. Mwenyekiti aliyokuwa akisema jana, amezungumza kati ya mambo ambayo yamefanywa mazuri zaidi katika Katiba Rasimu. Ukiangalia mfumo wa utawala, Rais ambaye tutamchagua kwa wakati huu hatakuwa tena Rais ambaye anaweza kufanya mambo bila kuhusisha wananchi. Ninakubali kuwa atakuwa Rais mwenye nguvu lakini kumewekwa vipengele mahususi vya kuhakikisha kwamba tena katika Kenya hakutakuwa mtu ambaye atakuwa na nguvu za kutawala na kufanya atakalo katika Katiba yetu mpya. Mtu akisema: Je, tukipitisha hii ni vizuri au la, una jibu lake. Tumeregesha tena senate ambayo Rais wa zamani kupitia chama chake cha KANU walivunja. Pia, walivunja sehemu za wananchi kujisimamia wenyewe kwa sababu ya kuongeza nguvu na mamlaka ya kati kati."
}