GET /api/v0.1/hansard/entries/111006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 111006,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/111006/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "kwa vile anajuana na Rais au wakuu wa Civil Service, anachaguliwa na kuapishwa kama hakimu. Baadaye Tume ya kupambana na ufisadi au the Kenya Anti-Corruption Commission (KACC) inasema kuna makosa yaliyofanyika na jaji huyo anasimamishwa kazi. Mambo haya yote yanafanyika chini ya Katiba ya sasa. Katiba hii mpya inatoa mamlaka kutoka kwa taasisi mbalimbali za Serikali na kuyaweka mahali pengine. Kwa mfano, the Judicial Service Commission (JSC) inapewa jukumu la kuwateua majaji chini ya Katiba hii mpya. This is superior. Hii JSC hapa ina nguvu zaidi kuliko vile ilivyo sasa. Hata katika kanda ya nchi za Afrika Mashariki, taratibu hizi za kuwateua majaji zimewekwa wazi. Ukiniuliza juu ya vipengele vya uteuzi wa majaji ni vipi vizuri katika Katiba ya sasa au hii mpya, hilo ni jukumu lako kuwamua wakati wa kura ya maoni. Mwananchi atapata nafasi ya kulijibu swali hilo. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati tunagawa pesa za Kenya kwa Wizara na maeneo Bunge mbalimbali, tunaona hakuna msukumo katika Katiba ya sasa wa kuhakikisha pesa hizi zinawafikia wananchi wetu mashinani. Wakati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha aliposoma Bajeti ya mwaka huu, alijaribu sana kuhakikisha kuwa pesa zilifika mashinani kupitia maeneo ya Bunge. Lakini jambo hili halijashughulikiwa vizuri katika Katiba ya sasa. Lakini Katiba mpya ambayo tunayoijadili wakati huu, haitakuwa na maoni ya Waziri wa Fedha kusema katika Bajeti hii tutatenga pesa kiasi fulani za kwenda mashinani kwa ajili ya miradi hii na ile, bali itakuwa ni lazima kufanya hivyo kuambatana na Katiba hii. Itakuwa ni lazima kutenga pesa fulani kwa ajili ya maendeleo mashinani. Mtu akiniuliza kati ya Katiba ya sasa na hii mpya ni ipi nzuri, swali hilo tulijibu wenywe wakati ufaao. Kipengele cha dual-citizenship au kuwa na uraia zaidi, kimepewa umuhimu katika Katiba hii. Ikiwa mtoto wako anafanya kazi nje ya nchi hii na anataka kuendelea kuwa Mkenya, basi Katiba ya zamani inasema jambo hili haliwezekani. Ni lazima ukiwa Mkenya ubaki Mkenya. Lakini Katiba mpya ambayo tunataka kupitisha inasema unaweza kuwa na uraia zaidi ya nchi yako ya Kenya. Kwa mfano, ukienda kutafuta kazi Afrika Kusini, Saudia au Tanzania na inakuhitaji kwamba kazi ambayo unayoifanya huko ni lazima uwe na uraia wa nchi hiyo, basi uraia wako wa Kenya haupotei. Ukiniuliza kati ya Katiba ya sasa na Katiba hii mpya tunayoijadili hapa, ni ipi nzuri, swali hilo nitakuwachia wewe mwenyewe kulijibu wakati wa kura ya maoni. Je, tukijadili maoni ya Kamati ya Wataalamu, Kamati ya Bunge na yetu sisi hapa Bungeni, tutakuwa tumepata Katiba ambayo haina hata dosari moja? Hilo ndilo swali ambalo ningelipenda tujiulize. Kamati ya kwanza ya Watalaamu ilitoa nakala ya Katiba ambayo ilikuwa na dosari fulani. Mwenyekiti wake, Bw. Nzamba Kitonga, alisema kuwa wao wameandika Katiba kielelezo lakini kuna maswala kadhaa wa kadhaa ambayo wangependa sisi kama Kamati ya Bunge kuyaangalia. Mimi nikiwa mmoja wao chini ya Mwenyekiti wetu Bw. Abdikadir na Naibu wake, Bw. Namwamba, tuliyaangalia mambo hayo yote kwa udani. Leo tumeyaleta mambo hayo yote kupitia kwa ripoti yetu hapa Bungeni. Kuna mambo mengine ambayo hatuwezi kusema ni kamili ndugu zangu. Mtu yeyote ambaye atakuja hapa na atoe mawazo yake pengine bora zaidi kuliko ya Kamati ya Bunge na yale ya Kamati ya Wataalamu, tusiwe na chuki naye, bali tuyaangalie kwa makini. Kama kuna maelewano kwamba kuna jambo ambalo ni lazima kuliangalie, ingefaa tuliangalie kwa makini. Hivi ndivyo tutaendeleza Katiba yetu. Ningependa kuwasihi wananchi wetu wakati wanapiga kura ya maoni, ikiwa kuna jambo mbaya zaidi ambalo tulilipitisha kama Kamati ya Bunge, Bunge au Kamati ya"
}