GET /api/v0.1/hansard/entries/111007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 111007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/111007/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "Wataalamu, basi tusikatae msimamo wa wananchi wetu. Sisi tumepewa nafasi nzuri zaidi ya kuwa na Katiba mpya. Sheria ambayo tumeunda sasa inatuelekeza njia hiyo ya kupata katiba mpya. Ndio, kuna hizi nafasi zote za kubadilisha na kuifanya hii Katiba iwe nzuri zaidi, lakini tusipoibadilisha nakala, itakuwa vyema zaidi kwa sababu ni nzuri hivi ilivyo. Tusiikatae na tusiwadharau wanaosema kuwa tuipitishe vile ilivyo. Lakini sio kusema kwamba yule ambaye ana wazo nzuri zaidi pia tumkashifu. Tusiwe na mioyo namna hiyo. Ninaomba tusikizane na tuelewane. Ikiwa kuna mtu ambaye atakuja na jambo nzuri zaidi, basi tukae tubadilishe. Lakini kama hatutaweza kupata nambari ya Wabunge thuluthi mbili, yaani 146, basi wananchi watukufu, Katiba ambayo tutaipitisha ni Katiba nzuri. Ni nzuri zaidi ya hii ambayo tumekuwa nayo kwa muda wa miaka mingi. Juzi wakati Rais wa Marekani alipokuwa akiipigia debe sheria juu ya mabadiliko ya afya au The Health Bill, alisema jambo ambalo ningelipenda kulizungumzia hapa kwa ufupi. Alisema kwamba Wabunge wa nchi yake walikataa kuogopa siku sijazo, wakazikumbatia. Katika Lugha ya Kiingereza alisema hivi: “We did not fear our future,we embraced it.” Tusiogope mambo yajayo, tuyaelewe na tuyakubali. Ni lazima tukubali kwamba Kenya imebadilika. Tunataka Rais na pia Bunge la Senate na Bunge letu la kawaida tofauti. Pia tunataka Judiciary tofauti. Tusiogope mambo yajayo, tuyakubali na kuyaelewa. Tusiwe na vita. Tupitishe Katiba Rasimu hii vile ilivyo ama kama mtu ataleta wazo njema zaidi, tuliangalie na kulipitisha kama Bunge."
}