GET /api/v0.1/hansard/entries/1111273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111273,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111273/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "speech",
"speaker_name": "Changamwe, ODM",
"speaker_title": "Hon. Omar Mwinyi",
"speaker": {
"id": 1345,
"legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
"slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
},
"content": " Asante sana, Bi. Spika Naibu wa Muda. Nitachukua muda mfupi kwa sababu wakati umeisha, kuwaunga mkono wanakamati waliokuja na Hoja hii. Na ziada ya waliotajwa ni Daktari wawili pamoja na Mhe. Sankok. Kusema kweli, shida ya hawa watu wazima au wazee ni kuwa sote tutakuwa wazee. Kwa ufupi, ni muhimu taifa letu liangalie maslahi ya wazee. Wengi katika ndugu zetu walio nje hutaka kuja kustaafu hapa, lakini huwa wanaogopa kwa sababu maslahi yao hayalindwi hapa. Pia, nashukuru shirika la APDK ambalo limeweza kuwaajiri robo tatu ya wafanyikazi wao kuwa watu ambao wana ulemavu. Itakuwa jambo la maana sana shirika kama hili likiungwa mkono. Nakumbuka Rais mstaafu Hayati Moi ambaye alichangisha tukapata majumba mawili, Rehema 1 na Rehema 2, ambayo yalikuwa ni ya kusaidia walemavu. Sijui kama pesa hizi bado zinasaidia walemavu ama vipi. Pengine Bunge hili lingeweza kuangalia swala hili. Vile vile, ningependa kuhimiza, tusiwafanye walemavu wetu kuwa ni waombaji. Kila mahali ukienda, waombaji ni walemavu. Pengine serikali za kaunti pamoja na Serikali Kuu zinastahili kutafuta namna ya kuwasaidia ili waweze kuchangia katika uchumi wetu. Kwa hayo machache na kwa sababu ya muda, napongeza Hoja hii."
}