GET /api/v0.1/hansard/entries/1111393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111393/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza ninawapa kongole walimu wa Kericho kwa kuleta malalamishi ya uandikishaji kazi na masaibu ya mishahara kwa walimu wa shule za chekechea. Tunaelewa kwamba shule za chekechea ndizo uti wa mgongo wa elimu ya watoto wetu. Kila mtoto anayezaliwa akifikia miaka mitatu au minne ni sharti aende shule ya chekechea ili awe na msingi mwema atakapoanza darasa la kwanza. Ni jambo la aibu hivi leo katika Kenya yetu. Jambo hilo haliko Kericho peke yake lakini katika kila mahali Kenya hii. Walimu wa shule za chekechea wanapata taabu sana. Wanabaguliwa na kutotiliwa maanani kabisa wakilinganishwa hata na wale wa darasa la kwanza. Mwalimu wa chekechea hatiliwi maanani kabisa katika shughuli zake za utendakazi. Tukiangalia katika serikali zetu za ugatuzi, walimu wanaoajiriwa na serikali na kufundisha katika darasa la kwanza hadi la saba wanaangaliwa vizuri na kulipwa mishahara. Wanaambiwa wao ni walimu wa kudumu watakaofanya kazi hadi kustaafu. Walimu wa shule za chekechea wanaweza kuajiriwa leo na baada ya wiki mbili, mwezi mmoja, sita ama kumi wakaachishwa kazi. Wanachukuliwa kuwa ni walimu wa rejareja tu hivi ambao hawana maana. Malalamishi haya yameletwa wakati mwafaka ambao Bunge la Seneti ni lazima litamke kupitia kwa Kamati yake ambayo itachunguza malalamishi haya. Tunaelewa kabisa ya kwamba katika utendakazi Wazungu walisema: “ A happy"
}