GET /api/v0.1/hansard/entries/1111742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111742,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111742/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Dullo, Seneta wa Isiolo. Shida kubwa ya vijana, hususan wale wanaotoka katika miji ya mipakani, ni kupata vitambulisho. Hii inatokana na sababu nyingi, mojawapo ikiwa wanatakinana kwenda vetting kabla ya kupewa vitambulisho. Vetting inatumiwa vibaya na wale wanayoifanya kwa sabau wanataka hongo kutoka kwa vijana ambao hawajapata vitabulisho na kazi. Kwa mfano, wengi wanaoenda vetting Mombasa wanasumbuliwa. Eti walete cheti zai ya shule, cheti cha kuzaliwa cha mzazi, mama au nyanya. Yote haya ni kujaribu kuwazuia kupata vitambulisho. Kitambulisho ni kitu cha muhimu sana kijana wa kike au kiume anahitaji ili aweze kupata ajira, masomo, na bursary ya kumwezesha kujiunga n chuo kikuu ama Technical and Vocational Education and Training (TVET). Hii ndio kila kitu. Hata kama anataka kwenda kufanya kazi nje, lazima awe na kiutambulisho ndio aweze kupata pasipoti ya kumwezesha kwenda kufanya kazi nje. Bw. Spika wa Muda, swala hili halijaletwa hapa kwa mara ya kwanza. Nilipokuwa katika Kamati ya Haki na Sheria, tuliangalia Ripoti ya IEBC kura ya mwaka 2017. Moja ya masuala illikuwa ni wangapi walikosa kupiga kura kwa sababu hawakuwa na vitambulisho? Ripoti ya IEBC ilipendekeza kwamba wakati wa kutoa vitambulisho iende sambamba na watu kuandikishwa kama wapigaji kura. Mapendekezo hayo"
}