GET /api/v0.1/hansard/entries/1111744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111744,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111744/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "hayajatekelezwa. Utaona vijana wengi ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na wanatosha kupiga kura wanakosa kujiandikisha kwa sababu hawana vitambulisho. Bw. Spika wa Muda, iwapo hawataandikishwa kwa sasa kama wapigaji kura wa mwaka ujao, watachukua miaka mingine mitano ndio waweze kupiga kura katika nchi hii. Hiyo ni kuwakosesha fursa ya kikatiba ya kuchagua viongozi ambao wanawapenda. Kamati husika ni lazima izamie suala hili kwa undani tuone ni sabau gani haiwezekani mashine za kutoa vitambulisho zipelekwa shule za upili ili wale wanaomaliza kidato cha nne wapewe vitambulisho vyao. Akitoka shule, anatoka na kitambulisho. Wale wanaofanya vetting katika mitaa waharakishwe wahakikishe kwamba wale wanaostahili kupewa vitambulisho wamepewa ili kila mtu ajihisi kwamba ni Mkenya kamili. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}