GET /api/v0.1/hansard/entries/1111778/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111778,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111778/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kwamboka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 9246,
        "legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
        "slug": "beatrice-kwamboka-makori"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninashukuru kiongozi wetu Sen. Dullo kwa kuleta Taarifa hii kwa wakati mwafaka. Wakati huu Wakenya wanahimizwa wajisajili kama wapiga kura. Ukweli wa mambo ni kuwa tumechelewa. Wizara ambayo inatakiwa kufanya mambo hayo inafaa kujuwa kuwa watoto wakiwa katika kidato cha nne huwa wamefikia miaka 18. Ni jukumu la Wizara kwenda katika shule na kuwasajili ili wachukuwe vitambulisho kwa sababu kila mtu ana haki. Bila kitambilisho mtu hawezi kuajiriwa kazi au kupiga kura. Wakati huu Serikali inawaambia wananchi waende wajisajili kuchukua kura. Ni jambo la kushangaza. Juzi nilienda katika ofisi ya chifu. Nilipata kuwa machifu ndio wanapigia wananchi simu waende kuchukua vitambulisho. Je, wakati hao vijana walikuwa wanajisajili kuchukua vitambulisho, hao machifu walikuwa wapi? Kama hizo fedha hazitoshi, mbona hiyo Wizara isitueleze sisi hapa tuweze kuongezea bajeti ili vijana wetu waweze kupata vitambulisho? Bw. Spika wa Muda, wakati mwingine vijana wanajisajili, wanaenda ofisini mwezi moja wakizungushwa. Kuna simu nilipiga wakati mmoja kwa ofisi ‘kubwa,’na hapo ndipo huyo kijana aliitiwa kitambulisho. Hiyo ni kama kuongeza ufisadi katika nchi yetu ya Kenya. Haya maneno yanafaa yaachiliwe kabisa na kila Wizara ijue ile kazi inafanya. Vijana wetu wachukue vitambulisho ndio waweze kupiga kura. Katika Jiji la Nairobi, watu 16,000 pekee ndio wamejiandikisha kama wapiga kura wiki iliyopita. Sisi kama vijana tunafaa tujitokeze na tujiandikishe kwa sababu inasemekana kuwa viongozi wanaowaongoza ni wabaya. Hapana! Kama wanataka kutekeleza demokrasia, waende wachukue kura na waje mwaka ujao wachague viongozi wanaotaka ama wafute kazi viongozi ambao hawafanyi kazi. Kwa hayo machache, nampongeza kiongozo wetu, Sen. Dullo, kwa kuleta hii Taarifa. Kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ya Usalama, tutahakikisha kuwa wale wanaohusika na maneno ya kusajili na vitambulisho watatueleza jinsi maneno yanafaa kuwa."
}