GET /api/v0.1/hansard/entries/1111782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111782,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111782/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "nimeshuhudia katika Kauti yangu ya Kwale, haswa sehemu ya Lunga Lunga ambayo ni mpaka baina na Kenya na Tanzania. Vijana wakienda kuchukua vitambulisho, wanaambiwa wapeleke hati ya kifo kama mzazi amekufa. Kama mama mzazi si mzima, wanaitishwa hati za familia mpaka uzeeni. Bw. Spika wa Muda, vijana wengi wanavunjika mioyo. Mimi nimeenda mpaka ofisi ya Kamishna wa Kaunti kule Lunga Lunga kuuliza ni kwa nini shida hii iko, haswa katika sehemu za mipakani baina ya Kenya na Tanzania, pale Vanga, Lunga Lunga, Jasini na Jego. Watu wakifika pale wakati wa uchunguzi utafikiri kunatolewa bursary . Wananchi hufurika pale wakingoja kuchunguzwa. Hili ni jambo ambalo chifu yuko pale, wazee wako pale, na ni kitu kinachochukua dakika mbili au tatu; kijana afanyiwe uchunguzi na apewe waiting card yake ndio achukue kitambulisho. Leo tumepata fursa kubwa kwa sababu tumeambiwa kwamba kama mtu hajajisajili kama mpiga kura na ana kitambulisho, ajitokeze kwa haraka aweze kujiandikisha. Lakini utakuta kuwa idadi ya watu inayojitokeza saa hii ni ya aibu. Wengi hawana vitambulisho. Watoto waliomaliza Kidato cha Nne mwaka jana au juzi, hawajapata vitambulisho. Watu pia hawaendi kuchukua vitambulisho vyao. Ukienda katika ofisi ya kusajili watu katika kaunti nyingi vitambulisho vimejaa. Mimi naonelea haswa machifu, naibu wao, Waheshimiwa Wabunge wa na sisi viongozi wote tuweze kuingia hizo ofizi za usajili ili hivi vitambulisho vipelekwe vijijini kwa haraka. Muda uliobakia ni mdogo sana, kama wiki tatu tumalize usajili wa kura. Kwa hivyo, Sen. Dullo mimi naunga Taarifa yako kwa sababu ni ya ukweli kabisa. Ile Kamati ambayo itaangalia hili jambo ifanye haraka sana."
}