GET /api/v0.1/hansard/entries/1111783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111783,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111783/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza natoa kongole kwa Sen. Dullo. Ameileta Taarifa yake kwa wakati mwafaka, hususan wakati wa kujiandikisha kupata vitambulisho na hatimaye kuchukua kura ili kuweza kupiga kura zao mwaka ujao. Bw. Spika wa Muda, sio Isiolo pekee yake ambayo shida hiyo imetokea. Ameleta hii Taarifa sababu katika Kenya mzima, kila mahali, kumeweza kuhusikana katika huu uandikishaji wa kura. Katika Kaunti ya Kilifi kuna vijana wa kike na kiume zaidi ya 5,000 ambao hawajaweza kusajiliwa kupata vitambulisho vyao, na hatimaye kuweza kuchukua kura. Shida inayotokea ni kwamba, walivyotangulia kusema wenzangu, kunazo kamati za wazee na kamati za machifu na manaibu wao ambazo zinakagua kama huyo mtoto ni wa eneo hilo. Utaona kwamba ukaguzi huo au kuangalia stakabadhi za watoto ambao hawakuweza kujitambulisha hapo zamani, hivi sasa wametegemea pengine zile stakabadhi zao za shule; imekua ni vigumu. Mara nyingi sio kwamba watu hawataki kujisajili kama wapiga kura, lakini kujiandikisha kupata vitambulisho kumekuwa kungumu sana. Kuna kizuizi kidogo au mvutano ambao unafanya wale wazee wapitishe zile stakabadhi kwa haraka ili vijana waweze kujiandikisha na kuchukua zile kadi zao ili wangojee vitambulisho vyao na baadaye wajiadikishe kupiga kura. Zoezi hili linachukuwa muda mrefu kwa sababu ya ukosefu wa kupitisha kwa haraka. Wale wazee au machifu ambao wanatakikana kusajili au kuwatambua hao vijana"
}