GET /api/v0.1/hansard/entries/1111785/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111785,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111785/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "wanaotaka kuchukua vitambulisho, ni vizuri ikiwa wao watafanya kwa njia ya haraka sana. Tunajua machifu wanaishi na sisi. Jambo la kusikitisha, kama waliotangulia kusema hapo awali, ni kwamba ikifika wakati wa kijana wa Kikristo hakuna shida. Inakuwa ni haraka sana kuweza kumsajili na kumwambia aendelee kuchukua kitambulisho chake. Lakini ikifika kusajili kijana wa Kiislamu ambaye pengine hakupata nafasi ya kwenda kusoma - amekuwa akisoma katika Madrassa au misikitini ama hakupata nafasi hiyo - inakuwa ni shida. Anaanza kuulizwa mama yake ni nani na kama aliwachana na babake. Itakuwa namna gan? Anaanza kuulizwa aseme babu yake ni nani. Anaambiwa alete hati ya kuzaliwa ya babu yake ama apeleke kitu chochote ambacho kinaweza kuonyesha mama au baba mzazi au jamii na ukoo wake. Wakati mwingine tunashindwa haya maswali yote yanahusikaje na usajili wa vitambulisho. Kama kijana ameishi na amezaliwa mahali fulani na tunamjua, hata kama mama yake aliolewa kwingine, haifai kumuuliza maswali mengine anapojiandikisha ilia apate kitambulisho. Haifa kumtesa kwa kumuuliza maswali, hususan kuhusu jamii yake na dini yake, alete kitambulisho cha mtu fulani na kadhalika, huu ni ubaguzi wa hali ya juu. Pia ni ukiukaji wa kuweza kutambua zile stakabadhi za wale vijana ambao wanataka vitambulisho. Ikiwa kijana ni Mkenya, amezaliwa katika eneo fulani, sio dini itamfanya apate kitambulisho. Hiyo ni haki yake kupata kitambulisho. Jambo la mwisho, hivi sasa, polisi wetu wafanye kazi za kutafuta na kuangalia amani katika nchi. Lakini, kwenda kujiweka mahali ambapo utaona kijana barubaru amekuja anataka kitambulisho na pengine mlikuwa na kesi naye ama mlikuwa mnamutafuta ama mulisikia, ndio sababu kunakuwa na uhaba wa vijana kujitokeza kujisajili kupata vitambulisho. Haya yanatendeka sana Kilifi. Tumesema ya kwamba kama ni namna hiyo, itakuwa vigumu sana kwa zoezi kama hili ambayo lina umuhimu fulani kufanyika, kwa sababu mwaka ujao watu watapiga kura na idadi ya watu watakaojisajili ili kuchukuwa vitambulisho itapungua. Bw. Spika wa Muda, zoezi hili linatakikana liwe huru iwezekanavyo kwa sababu tunajua katika sheria kupata kitambulisho cha kuenda kupiga kura, ukijisajili na upewe kura yako, ni haki yako kuenda kupiga kura na kumchagua yule ambaye unataka apite katika ile kura. Hiyo ndiyo itakuwa ni muhimu sisi kuwaambia Wakenya. Wakati umefika sasa. Wakenya wote wajiandikishe na wale ambao hawana vitambulisho wazichukue. Wale ambao kura zao zimepotea pia wako na wakati wa kujiandikisha ili wapate vitambulisho vya kura. Wale ambao hawajajiandikisha, kwa mfano vijana, tunawahimiza--- Mimi kama Seneta wa Kilifi, nitawaambia vijana wa Kilifi wachukue kura kwa wingi kwa sababu sisi tuko na kura nyingi. Tuko na kura zaidi ya milioni moja na nusu na sasa tunataka kufikisha milioni mbili. Kwa hivyo, tunahitaji vijana wachukue kura na wajitayarishe kupambana na kivumbi kile kitakachokuwa mwaka 2022. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}