GET /api/v0.1/hansard/entries/1111795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111795,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111795/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nizungumze machache kuhusiana na taarifa ambayo imeletwa na Sen. Dullo. Kwanza, nataka kumpongeza kwa kuleta taarifa hii kwa wakati huu. Huu ni wakati mwafaka na imekuja wakati ambao unafaa. Unapozungumza mwisho huwa mengi yamezungumzwa lakini kuna mengine ambayo nitasisitiza. Inasemekana kuwa kitambulisho ni haki ya kila mtu, nami pia naamini hivyo. Kuna masuala ambayo yanazungumziwa ambayo nitayazungumzia, kuhusu usajili wa vitambulisho. Wakati mtu anasajiliwa ama ameenda kusajiliwa, yale maswali yanaoulizwa yanaudhi. Wakati mwingine wale ambao wanahusika kwa usajili wanaandika majina yakiwa na makosa ambayo yanaleta shida baadaye. Kwa mfano, mamangu alikuwa akiitwa Jumwachengo lakini kitambulisho chake kilikuwa kinasema Jumwarija, hiyo ‘chengo’ ilikuwa imeendikwa ‘rija’ ilikuwa shida sana. Akajaribu kubadilisha lakini kitambulisho kilipokuja kilikuwa na makosa tena. Nawasihi wanaohusika na uandikishaji wa vitambulisho, wawe makini sana ili majina yawe sahihi. Kule kwetu utakuta mtoto anaitwa Joseph Charo, anaandikwa Joseph Kyalo na sisi hatuna ‘Kyalo’ kule kwetu. Tuna ‘Charo’ Inabidi tena baadaye arudishe kitabulisho ili kirekebishwe jina tena. Siku ya kuzaliwa inaandikwa makosa pia. Juzi nilisafiri halafu katika ile hali ya kutaka kutoa pesa na nimezoea kutoa na M-pesa nikawa nimesahau PersonalIdentification Number (PIN) yangu ya bank. Mwisho nikablock ile kadi yangu ya benki. Niliporudi Kenya nikataka k uactivate – poleni nitazungumza sijui maneno mengine kwa Kiswahili – kadi yangu ya benki . Kila nikijaribu inaniambia siku yako ya kuzaliwa haiambatani na ile siku ambayo iko hapa. Kwenda benki nikawaelezea siku yangu ya kuzaliwa, wakaniambia siku umesema hapa siyo ambayo iko hapa. Ikabidi nitafute kitambulisho. Nilipopeana kitambulisho, nilikuwa nimepoteza kitambulisho hapo nyumaye kwa hivo nikawa nimebadilisha kitambulisho kingine. Nilipopeana kumbe walibadilisha wakaandika tarehe ambayo si yangu ya kuzaliwa. Hiyo ingekuwa shida lakini benki walinielewa kwa vile mimi ni mwenyewe na wana picha yangu. Kwa hivyo, wanaohusika na usajili wa vitambulisho wawe makini. Kule kwetu hatuna Kandzo Mwende tuna Kandzo Mwenda, tuna Mwenda sisi na si Mwende. Kuna Watoto kule kwetu mpaka sasa wanaitwa Mwende. Wale wahusika watakuwa wanaandika ama kuajiri watu wa kusajiri wahakikishe wanaajiri watu wa maeneo hayo. Hata kama watakuwa wawili watatu ambao mtu akisema jina ni rahisi mtu kuelewa anasema jina gani. Mara nyingi majina yamekuwa shida kwa kutamka. Upande wa usajili, kuna wakati nilikuwa nataka pasipoti na nikaenda kwa ofisi ya usajili ya vyeti vya kuzaliwa. Nilipofika pale nilipata shida kwa kuwa mamangu alikufa"
}