GET /api/v0.1/hansard/entries/1111797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1111797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111797/?format=api",
    "text_counter": 93,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "zamani na nikaambiwa nikatafute cheti chake cha kuzaliwa ambapo hakuwa nayo. Mimi sikuwa na cheti hiyo na hata yeye hakuwa nayo. Hii ndio maana nikawa nimeenda kutafuta cheti cha kuzaliwa kwa sababu nilikuwa nataka kupata pasipoti niliambiwa ni lazima niwe nayo. Kwenda pale nikaambiwa nipeleke cheti ya kuzaliwa ya mamangu na alikufa zamani na alikuwa hana cheti hiyo. Nitaipata wapi? Baadaye nikaambiwa nitafute kitambulisho chake, sijui kilipotea vipi kwa kuwa mamangu alikufa kitambo nikiwa mtoto mdogo. Nikaenda kwa chifu kwa kuwa tunajuana na yeye - naenda hapo kwa sababu amezungumzia Sen. Omogeni kuhusu machifu - aliandika barua kwamba mamangu ni fulani na kuelezea ukoo wetu wote ndio mwisho nikapata huo usajili. Kuna maswali mengine ambayo yanaudhi. Siku hizi muundo wa Serikali naupenda kwa sababu imeleta watu wa nyumba kumi. Kama watu wa nyumba kumi wako, ni kidogo ambazo yule mzee ana uwezo wa kujua kila nyumba ina watu wangapi na ni mtoto gani amezaliwa. Inafanya huo usajili uwe rahisi. Mpaka sasa ni shida, unatoka kwa chifu, Deputy County Commissioners,County Commissioners, mzee wa Kijiji mpaka mzee wa nyumba kumi. Serikali imeleta huduma mashinani kabisa. Iweje tena kama unataka kitambulisho mpaka ujibu maswali mengi?"
}