GET /api/v0.1/hansard/entries/1111798/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111798,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111798/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, kuna huu ugonjwa wa UKIMWI ambao ulikuja. Watoto wengi wameishi hawana wazazi, kabla dawa za kuua UKIMWI ndio uishi kwa siku nyingi, watu wengi walikufa wakati ule. Watoto wengi ni mayatima, wanaishi na nyanya zao ambao walikuwa wazee na pengine walikufa. Ukienda kumuuliza maswali mtoto kama huyu hajui akwambie nini, mamake, babake na nyanyake hakumuona. Tukitaka taarifa ya huyu ni tujue kwa mzee wa kijiji ama mzee wa nyumba kumi ambaye ana taarifa ya mtoto alipozaliwa. Hospitalini kazi imekuwa rahisi. Kwa sababu watoto wangu wote nimewazalia hospitali naezaenda na kuuliza stakadhabi zake zote za mtoto wangu kuzaliwa. Iweje mtoto akitaka kitu mpaka aulizwe maswali? Tuko kwenye ulimwengu wa kidigitali sio wa zamani wa kutapatapa. Kuna mahali wanaweka vitu vyetu, ukigonga tu vinajitokeza vyote. Mkatuletea huduma namba, mkasema ukipewa basi mambo yako yote yanaishia pale. Sijui ama ni kweli ama ni kitendawili? Nikiitishwa kitambulisho huwezi wapatia huduma namba . Kumaanisha inahudumia mambo mengine na kitambulisho mengine. Nasihi wanaohusika na usajili wa vitambulisho wafanye usajili kwa makini. Sisemi wasiulize maswali lakini waulize maswali ambayo yanahitajika. Kuna maswali mengine ambayo yanafanya vijana wanahofu kwenda pale. Wanaulizwa maswali ya aibu mbele ya watu. Unamuuliza ‘babako ni nani?’ Watoto wengi tusifichane, hawana wazazi wa kiume. Poleni wanaume mko hapa na pengine wananisikiza lakini wameacha majukumu yao. Majukumu mengi huchukuliwa na mama. Ukiuliza babako ni nani mbele za watu na ameishi akiwa na mama unamwaibisha. Tafuteni maswali mazuri ya kuuliza, mtafanya watu wengine wasichukue vitambulisho waogope ilhali ni haki yao kuvichukua. Hatuna makosa sisi, Mwenyezi Mungu ametupa mimba, tumezaa na tunalea watoto. Hiyo isiwe hali ya nikizaa mtoto aishi kama ambaye ana ulemavu kwa sababu hana baba. Mtoto yule si mlemavu ana haki zote za mtoto wa kawaida, ashughulikiwe."
}