GET /api/v0.1/hansard/entries/1111800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1111800,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1111800/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Haya maswali mtakayouliza muulize maswali ya hadhi na mtoto hatajihisi kwamba amebaguliwa na kutengwa katika jamii. Naunga mkono Statement ambayo imeletwa na kuna zile hatua ambazo zinafaa kuchukuliwa ili watu watajitokeza kwa wingi na kuchukua vitambulisho. Nasihi Kenya nzima na Kaunti ya Kilifi ambako natoka, kuna wakati kulikuja Mswada hapa Bunge, ni vile haukupita, kwamba shilingi moja, mtu moja, one man one vote one shilling. Bw. Spika wa Muda, kusema kweli, kama Mswada huo ungepita, sisi watu wa Kilifi tungekuwa na shida sana. Hii ni kwa sababu tuko wengi, lakini wengi bado hawajachukua vitambulisho. Kwa hivyo, inakuwa shida kupiga kura kwa wapigaji kura. Huwezi kupiga kura kama huna kitambulisho. Mimi nawasihi Wakenya wote, na nina sisitiza kwa watu wa Kilifi kuwa ni haki yao kupiga kura. Miswada huu haikupita juzi wala jana, lakini huko tuendako hatujui kama Mswada kama huu utakuja upite. Ukipita, tutakuwa kwa shida kwa maana Mswada huo utakuwa hautufai sisi hata, na hatutakuwa na la kufanya. Kuzuia mambo kama haya yasitokee, ama hata yakitokea tusikue na shida kwa sababu tumejipanga kisawa sawa, tuchukue vitambulisho ili wakati wa kupiga kura ukifika, tupige kura kwa wingi. Asante, naunga mkono."
}