GET /api/v0.1/hansard/entries/1112156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1112156,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1112156/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi nami nichangie. Naunga mkono ombi la sala za kitaifa. Mhe. Spika, shida ya Kenya ni kwamba tunaenda misikitini na makanisani kwa wingi lakini roho zetu haziko safi. Kwa hivyo, tunahitaji Mwenyezi Mungu aongoze hizi nyoyo zetu ili yale tunayokwenda kusema na kufanya yawe ni hayo hayo, haswa wakati huu wa karibu na uchaguzi, shida inakuwa kubwa Kenya. Tunahitaji maombi maana kuna viongozi na wanasiasa kama sisi ambao wengine wataona wako mbele na kumbe wakija wakiona uchaguzi sivyo walivyotarajia, italeta shida. Kwa hivyo, tunahitaji maombi. Maombi ni muhimu. Nchini Kenya hatuna shida ya sheria wala mambo mengine. Shida ni hatuna uadilifu. Kwa hivyo, tunahitaji Mwenyezi Mungu atuongoze."
}