GET /api/v0.1/hansard/entries/1112645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1112645,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1112645/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Wengine waliuza mifugo na mashamba yao ili kufanya kadarasi ya Serikali. Ni uchungu sana kwa sababu mpaka siku ya leo hawajapata pesa zao. Utakuta wengi wao wamekaa katika majengo au ofisi za kaunti wakidai pesa zao na hawajui watalipwa lini. Mambo haya ni mazito siyo ya kuchukulia rahisi. Ikiwa kandarasi ya Serikali itafanya watu wetu wakuwe maskini na wawe hohe hahe, basi watu hawataweze kuendelea kuishi katika hali hii ngumu iliyojaa shida na uchungu mwingi. Jambo hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito ili suluhisho la kudumu lipatikane."
}