GET /api/v0.1/hansard/entries/1113245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1113245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1113245/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nominated, FORD-K",
    "speaker_title": "Hon. Nasri Ibrahim",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi. Watu wa Kaskazini Mashariki na wafugaji kwa ujumla wameteseka kupitia ukame huu. Wakazi katika sehemu hizo hutumia mifugo kama tegemeo lao. Huuza mifugo yao sokoni ili wapate fedha za kununulia chakula, na pia kwa kukamua maziwa. Tangu ukame umalize mifugo, wanateseka na njaa na ukosefu wa maji. Mifugo wamekufa kwa ajili ya kukosa malisho na maji. Serikali za kaunti zimejaribu kuwachotea wananchi maji ili waweze kuokoa mali yao. Hata hivyo, serikali za kaunti pekee haziwezi kutosheleza mahitaji ya wakazi katika kaunti nzima ama wafugaji wote vile inavyotakikana. Hata wanyamapori katika maeneo kame wamekufa kutokana na ukosaji wa maji. Ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii, utaona pia wanyamapori wakipewa maji na wananchi. Raia wakikosa vitu vya kula, watakufa kutokana na njaa. Naiomba Serikali Kuu ijitokeze haraka walete msaada wa dharura ili tuokoe maisha ya watu wetu. Hii ni kwa sababu, wanapopoteza mifugo kupitia kiangazi, hawana namna ingine ya kujisaidia kimaisha. Watoto pia hawaendi shuleni kwa sababu wazazi wamebaki kwa vyumba. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu."
}