GET /api/v0.1/hansard/entries/1114986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1114986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1114986/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Mhe. Spika, hii ni jambo la kusikitisha ambalo halieleweki kwa sababu ardhi hii inahistoria kuanzia mwaka wa 1830 na kunajulikana watu walikuwa hapo kuanzia mwaka 1927. Kwa niaba yangu, Marehemu Mzee Shariff Nassir, aliyekuwa Mjumbe wa Mvita na baba yangu, ni mmoja wa walioweka jiwe la msingi la kujenga msikiti katika eneo hio mwaka wa 1980. Leo hii, mtu amekuja kutoka Nairobi na kuambiwa atapatiwa Title Deed ya msikiti ule. Wakaazi walio pale ni 12,600 na hatuwezi kukubali mwenendo huu. Hawa ni watu walio na hamu ili Serikali iweze kuwatolea fidia na huyu mtu hakutoa jasho lake wala kufanya jambo lolote. Sio hapa pekee, hata kule Mvita nimeweza kupeleka ombi kwa National Land Commission (NLC) na wakatoa raslimali inayofaa kulipwa ambayo nitaleta rasmi katika Kamati. Asante sana, Mhe. Spika."
}