GET /api/v0.1/hansard/entries/1114990/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1114990,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1114990/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili nami niweze kuchangia. Wenzangu wamezungumza juu ya Ardhilhali tatu ambazo zimeletwa hapa. Lakini, mimi nitazungumzia Ardhilhali ya Mhe. Mishi, Mbunge wa Likoni, juu ya watu wa Mwananguvuze. Mhe. Spika, haiwezi kuwa kuanzia mtu mmoja mpaka wakafika watu12,000 na mtu huyu hata hajui historia ya ardhi ile na anatakakuinunua. Kwa hivyo, ni muhimu Serikali hii iwezekuona kuwa mambo haya ya watu kuhamishwa kiholela yamekomeshwa. Mimi nampongeza Mhe. Mishi kwa sababu tumekuwa na yeye kutoka Bunge la 11, na wakati huo alienda kwa NLC mara mbili kuwatetea watu wale. Akifanya hayo wakati huo, nami nilikuwa nawatetea watu wa Aldina kutoka eneo Bunge langu la Jomvu. Kwa hivyo, watu 12,000 hawana mahala pengine pa kuishi, hapo ni kwao na hawawezi kuenda Uganda au Rwanda. Hapo ndipo walizaliwa, mahali ambapo kuna misikiti, makanisa na shule. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}