GET /api/v0.1/hansard/entries/1114996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1114996,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1114996/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "umasia",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kule Kiambu. Kwa kweli, hili Bunge linapaswa kuamka maanake kwa sasa, maswala kama haya haliwezi kutofautisha kama ni mtungaji sheria, mzalishaji au yule anayekula. Mhe. Spika ukiniruhusu, kwa Kiingereza, ni consumer politician and producerpolitician . Kenya tunaelekea mahali ambapo si pazuri, kama maswala ya vyakula vya mifugo vitaendelea namna hii. Pia, naunga mkono Ardhilhali ya pili na ya tatu, yale ya kwa Kazengo na vile vile, haya ya Mwananguvuze. Haya malalamishi ni mengi sana nchini Kenya. Juzi tu, kule kwangu, nimeshangaa watu walioishi zaidi ya miaka 20 na, wanafurushwa na Shirika la Wanyama Pori. Hii miaka yote, wamekuwa wapi wakigojea watu wajenge hapo. Kamati husika linapaswa kuchunguza maswala haya kwa undani na wayatatue haya malalamishi kwa haraka, angalau wananchi wanaoishi kule wasaidike. Katika eneo Bunge langu, sehemu ya Maungu, watu zaidi ya 500 wamefurushwa kama wiki tano au sita zilizopita. Wote wanakimbia kulalamikia viongozi wao na ukiangalia hela ilivyo kwa sababu ya huu ugonjwa wa Korona, kuna matatizo mengi sana. Kwa hivyo, Kamati husika inapaswa kuamka na ile Kamati tekelezi isilale lakini iyende mbio ndiyo maswala kama hawa yamalizike. Asante sana, Mhe. Spika."
}