GET /api/v0.1/hansard/entries/1115660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1115660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1115660/?format=api",
"text_counter": 341,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Nasema kulingana na Kipengee 41(5) cha Katiba ambacho kinasema juu ya mambo ya jumuiya mataradhio, yaani collective bargaining, kuwa watu wana haki ya kuona ni vipi wanaweza kukaa na kukubaliana. Kwa hivyo, kwa dakika mbili ulizonipa, nataka kusema kuwa ni muhimu Kamati Tekelezi au Implementation Committee ifanye haraka iwezekanavyo kuchukua mapendekezo ya hii Kamati na kuona kuwa watu wa KPA wamelipwa. Vilevile, tunasema kuwa, kibinadamu na wakati huu mgumu wa Korona, watu wote waliofutwa waregeshwe kazini ili wajikimu na kujimudu katika maisha yao kama kawaida."
}