GET /api/v0.1/hansard/entries/1115665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1115665,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1115665/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Kwanza, nataka kutoa shukrani na kongole kwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya Leba na Ustawi wa Jamii. Pia namshukuru Mhe Abdullswamwad kwa kutetea wafanyikazi wa bandari ambao ni vijana wetu, akina mama na akina baba. Kwa hakika Kamati imeangalia sheria kwa sababu sheria ni msumeno. Yakata mbele na pia yakata nyuma. Wafanyikazi wa bandari wamekuwa wakichangia Hazina Kuu ya taifa na uchumi wa taifa letu la Kenya pakubwa sana. Wafanyikazi hawa, mbali na kuwa kulikuwa na Covid-19 ama Korona, walimenyeka na kung’ang’ana kabisa kuzalisha na kuhakikisha kwamba mapato ambayo yanaingia katika Hazina Kuu ya taifa hayakupungua wala kuwa machache kwa sababu ya Korona. Wafanyikazi wa bandari wanafanya kazi katika hali ngumu na hatari pale bandarini. Kwa hivyo, watu walikubaliana katika mjadala wa pamoja na dock workers na KPA wakaweka kidole kusema “tunaweza kuwapa mishahara na posho zao na wala haitaathiri ule uchumi tunatengeneza pale katika bandari”. Kwa hivyo, iwapo bandari imesema inaweza, kwa nini SRC iseme haiwezi na wale KPA wanajua mapato wanayopata na wafanyikazi wao? Jambo jengine, wafanyikazi 247 ni familia 247 wakiwemo akina mama, watoto na watu wengi. Sisi kama Wakenya na viongozi tuhakikishe kwamba wameregeshwa katika kazi zao ili waweze kusomesha watoto, kujenga taifa na kuwa na maisha ya Wakenya ambao wanaheshimika."
}