GET /api/v0.1/hansard/entries/1116280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1116280,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1116280/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Namshukuru Mwenyekiti, Mhe. Kareke Mbiuki. Vile vile, namshukuru Naibu wake, Mhe. Sophia Abdi. Kama alivyosema Mwenyekiti, Mhe. Kareke Mbiuki, nimeridhika kama Mbunge wa Jomvu. Mradi wa Danaff uliokuwa ufanyike ulimalizika mwezi wa Agosti. Vile vile, tuko na cubicmetre 4,000 ambazo tutawapatia wananchi wetu. Kitu ambacho ningetaka kuzungumzia ni kuwa haya majibu si ya leo pekee. Mhe. Mwenyekiti alifanya kikao na officials wa Wizara, Mkurugenzi wa Coast Water na mimi. Kama alivyosema, aliwaamrisha wawasiliane nami. Naripoti kuwa wiki ijayo, nitakuwa na mkutano na Mkurugenzi wa Coast Water na Mkurugenzi wa Mombasa Water, Bwana Carmel Bokoko, kuhusu mambo haya ya Jomvu. Inasikitisha kwa sababu ni hujuma na usaliti mkubwa sana kuona maji yakitoka Mzima, yapite Mazeras, yaanze katika Kaunti ya Mombasa kwenye Eneo Bunge langu la Jomvu, yaende mbele mpaka Mombasa Mjini na watu wangu wakose maji. Lakini tangu Mwenyekiti na Naibu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}