GET /api/v0.1/hansard/entries/1116884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1116884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1116884/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kwanza, nataka kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa na Kamati ya Fedha ya Mipango ya Kitaifa, ikiongozwa na Mhe. Gladys Wanga. Ripoti hii imetuonyesha kwamba katika Kenya hii, asilimia 50 ya bei ya mafuta inategemea bei ya dunia nzima na pia tumeona asilimia 50 nyingine ni ushuru ambao Kenya yetu inatoza bidhaa ya mafuta. Linalonitia wasiwasi ni kuwa tumekuwa katika kipindi kigumu cha COVID-19 ambacho Wakenya wamekuwa na changamoto chungu nzima. Mwaka jana, tuliona Serikali ikijitokeza kidete na kusema kwamba itaanzisha mpango wa kupunguza gharama ya maisha kwa wananchi lakini bidii hiyo yote Serikali imeweka imeweza kupotea kwa sababu bei ya petroli ilipopanda mpaka Kshs136 na mafuta ya taa kufika Kshs10, Wakenya wengi wamepatikana katika hali yakuwa maskini zaidi. Wameshindwa kufanya biashara zao katika hali ya kawaida. Waendeshaji wa boda boda leo hii wanashindwa hata kupandisha bei ya usafiri kwa sababu Wakenya wanakosa pesa ya kuwawezesha kusafiri wanavyotaka. Kamati hii imetujulisha mambo mengi lakini la msingi ambalo latakikana Kenya na Wakenya wote wajue ni kwamba tunapofanya bidii yakushukisha mafuta, lazima tuangalie ushukishaji huo usiwe kama kupamba Wakenya tu au kuwapaka Wakenya mafuta kwa mgongo wa chupa. Ile pesa ambayo yasemekana mafuta yatashuka ni karibu Kshs10 peke yake. Kwa kweli Kshs10 ni asilimia ndogo sana kuangalia vile bei ya mafuta ilivyo sasa. Mimi binafsi na wale Wakenya ninaowasikiliza wanasema kama kweli sisi ni wawakilishi wao na tuna uchungu wanaoupitia Wakenya; lazima Bunge hili la Taifa lisisitize kwamba bei ya mafuta ni vyema ishuke kwa zaidi ya asilimia 30 au ikiwezekana asilimia 40. Kuna wakati bei ya mafuta ilikuwa Kshs70. Wakati ule, Wakenya walikuwa wanaweza kufanya biashara zao bila wasiwasi. Sasa kutoka Kshs70 imeenda karibu mara mbili hadi Kshs136, halafu tunasema ipungue tu kwa Kshs10 au Kshs12. Kweli tutakuwa hatujafanya la msingi ambalo Wakenya wengi wanatazamia. Kuna jambo lingine tena limeibuka kuwa huu ushuru tunaotoza mafuta uko mwingi sana mpaka Wakenya wanaofuatilia masuala haya wanashindwa ni vipi product moja ambayo ni mafuta inaweza kutozwa ushuru wa viwango tofauti. Sasa tunasema ingewezekana kama ni VAT, tulisema katika Bunge hili na wengine wametaja miaka miwili iliyopita na Mhe. Naibu Spika wa Muda ulikuwa umeketi katika Kiti hicho… Tulipiga nduru sana katika Bunge hili ili mafuta yawe"
}