GET /api/v0.1/hansard/entries/1116982/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1116982,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1116982/?format=api",
    "text_counter": 354,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lari, JP",
    "speaker_title": "Hon. Jonah Mwangi",
    "speaker": {
        "id": 13405,
        "legal_name": "Jonah Mburu Mwangi",
        "slug": "jonah-mburu-mwangi"
    },
    "content": "wapata biashara, kesho wapata hasara, kesho wapata faida. Lakini pale twaona mafuta watu wapata faida kutoka Januari mpaka Disemba. Kule kwetu raia wananung’unika kila siku, wamekatazwa leseni za kuvunja kuni kule msituni. Kila siku wanalia, “Mheshimiwa tusaidie tuvunje kuni”. Kwa nini tusipunguze ule ushuru wa LPG uwe zero ndio tuencourage nchi yetu kuwa na clean gas, tuwe tunapika na hewa safi, tunapika na ile hewa ambayo inakuwa imported? Na pia, kwa yule mtu ambaye yuaimport, ile soko ifunguliwe tusikuwe ati ni mtu mmoja tu 90 per cent ambaye yuaimport zile LPG. Hii nchi yetu ni kubwa sana. Wawekezaji ni wengi. Kwa hivyo, lazima tupunguze. Sababu ingine ya kupunguza bei ya mafuta ni nini? Kila siku twaambiwa stima yetu iko ghali kwa sababu ya gharama ya mafuta. Kwa nini tusipunguze ile tax ya mafuta ndio stima yetu ikuwe bei rahisi na wawekezaji waendelee kuja Kenya, waendelee kuweka viwanda, nao watumizi wakuwe wengi? Watumizi wakitumia twapata tax kwa njia nyingine ambayo itakuwa nyingi tena zaidi. Mimi nahuzunika. Mimi nasononeka nikiona jinsi mwananchi yuaumia kila siku. Mwananchi yuaumia juu ya nini? Ni kwasababu tunakosa kuwapea maadili mzuri ya kufanya kazi ya mafuta. Kwa hayo mengi na machache, Mheshimiwa mwenzangu hapa amelia sana ati hajapata nafasi. Ni Mheshimiwa kutoka Samburu West. Nakuombea nafasi tafadhali. Nashukuru Madam Spika lakini umsaidie huyu Mheshimiwa. Nashukuru Madam Spika na ninasupport ule mjadala."
}