GET /api/v0.1/hansard/entries/1119388/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119388,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119388/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyoletwa na Senata wa Narok, Sen. Olekina. Ni wazi kuwa Serikali ya Kenya haina hamu ama haina nderemo ya kupambana na ufisadi. Kwa sababu kutoka Rais alipotoa maagizo kwamba uchunguzi ufanywe kuhusiana na sakata ya Kenya Medical supplies Authority (KEMSA) mpaka sasa hatujaona ripoti yoyote. Tuliambiwa faili ilipelekwa kwa Director of Public Prosecutions (DPP) na ikaregeshwa kufanywa marekebisho na mpaka sasa hakuna yeyote ambaye amepelekwa mahakamani kuhusiana na kashifa hii. Bi Spika wa Muda, wafanyaji kazi wadogo sasa wako hatarini ya kupoteza kazi yao kwa makosa ambayo sio yao. Makosa haya yamefanywa na watu wengine ambao ni wakubwa katika shirika hilo na ambao kwa sasa wametolewa kwenye KEMSA, wakapelekwa sehemu zingine na wanaendelea kazi zao na maisha yao kama kawaida."
}