GET /api/v0.1/hansard/entries/1119523/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119523,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119523/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bwana Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Ajira na Huduma za Jamii. Jana nilikatizwa nilipokuwa natoa sababu za kutokuwa na ufahamu baina ya waajiri na wale wafanyi kazi ambao wanatoka hapa Kenya kuenda kufanya kazi kule Saudi Arabia na kwengineko. Lugha ni jambo ambalo linaleta shida baina ya wafanyikazi na waajiriwa wao. Waajiri wengi wanatumia lugha ya Kiarabu na Wakenya wengi wanatumia Kiingereza, Kiswahili na lugha zao za mama. Kwa hivyo, mawasiliano baina ya muajiri na mfanyajikazi wake inakua ni shida. Kitu kingine ni kwamba hakuna mafunzo wanayopewa wale ambao wanasafiri kuenda sehemu zile kabla ya kuenda kuanza kazi. Ni muhimu wapate mafunzo ili wajue matarajio ya muajiri wao na matarajio yao katika hiyo kazi. Hiyo imeleta shida. Watu wengi wanaenda hizo sehemu na hiyo imechangia kuongezeka kwa malalamiko. Jambo ambalo ningependa kusema ni kuwa wale ambao wanapata matatizo ni wachache kuliko wale ambao wanafanya kazi bila matatizo yoyote. Ni muhimu hiyo ijulikane ili isije ikaonekana ya kwamba watu wote wanao kwenda kufanya kazi sehemu zile wanateswa, wana nyimwa mishahara, wanazuiliwa kupata uhuru wa kuenda kutembelea jamaa zao na kadhalika. Ni wazi kwamba wengi wanaofanya kazi kule wanafurahia kazi zao na ndio maana kila mwezi ama kila mara wanatuma fedha kwa jamii zao. Mwezi uliopita; Mwezi wa tisa, nilikabidhiwa matatizo ya mmoja kati ya wafanyikazi ambao wako kule Saudi Arabia anayeitwa Karen. Familia yake mjini Mombasa ilinijulisha kwamba Karen yuko Saudi Arabia na anafanya kazi kule lakini anateswa. Yeye pia alinitumia text kupitia kwa Whatsapp akanieleza masaibu yake. Alinipa namba ya ajenti wake anayejulikana kama Issa ambaye yuko hapa Nairobi. Nilitumia Issa ujumbe na ningependa kunukuu vile ambavyo tuliwasiliana naye. Nilimtumia ujumbe nikamwambia, „huu ujumbe unatoka kwa bibi mmoja anayeitwa Karen na nimetumiwa na jamaa zake.‟ Aliniuliza, „shida yake ni nini?‟ Nilimwambia shida ni kwamba anasema anateswa na anafanywa kama mtumwa kule anakofanya kazi. Majibu yake yalikua ifuatavyo. „ What is she subjected to? Amefungwa na chains?’ Nilimwambia „la, hajafungwa na nyororo lakini mimi kama Seneta wa Kaunti ya Mombasa ningependa kujua matatizo ni nini ili tuweze kumsaidia.‟ Majibu yake yalikua kama ifuatavyo, ‘if you are indeed a Senator, why can you"
}