GET /api/v0.1/hansard/entries/1119532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119532,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119532/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Singependa kuchukua muda mrefu kuweza kunukuu maneno hayo, lakini hayo ndiyo majibu ya wale mawakala ambao wanapeleka wafanyikazi hawa katika sehemu zile za nje kwenda kufanya kazi. Tunaweza kulaumu watu wa Saudi Arabia, United Arab Emirates (UAE), au Qatar, lakini papa hapa kwetu hiyo ndiyo attitude ya hawa wanopeleka wafanyikazi hawa. Huo ndio utendakazi wao, kwamba hawako tayari kusikiliza malalamiko ya wafanyikazi ambao wao wenyewe wamewepeleka kwa kulipwa. Mheshimiwa Spika wa Muda sio rahisi msichana ambaye amepelekwa sehemu zile kwenda kufanya kazi aweze kukataa kufanya kazi. Hii ni kwa sababu anajuwa amekwenda kufanya kazi na anatarajia malipo ya kazi ile. Hawaendi kule bure. Kila dalali analipwa sio chini ya Kshs100,000 kumpeleka mtu mmoja kwenda kufanya kazi kule. Tatizo kubwa liko katika madalali wetu. Hawa mawakala ambao wanachukua hawa wasichana kwa ajira katika sehemu zile wanafaa kukabwa zaidi kwa kupewa vigezo vigumu vya kutekeleza kabla ya kupewa ruhusa ya kuweza kupeleka wafanyaji kazi katika sehemu zile. Itasaidia pakubwa kuondoa tatizo hili. Ikiwa wakala majibu yake kwa Seneta ni haya, utafikiria majibu kwa yule mfanyikazi ambaye yuko kule yatakua namna gani? Na yule mfanyikazi hajui mtu mwingine ambaye yuko naye kule isipokuwa wakala wake. Hata familia ikienda kudai, katika hawa mawakala, utapata kwamba wengi wanajibiwa majibu ya ovyo. Wana tukanwa kwa sababu wamempa wakala kazi ya kupeleka mfanya kazi katika sehemu za Ughaibuni kwenda kufanya kazi. Kazi ile imemsaidia wakala na vile vile familia ya yule mhusika."
}