GET /api/v0.1/hansard/entries/1119536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119536,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119536/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Singependa aniarifu kwa sababu inahitilafiana na mwongozo wangu ambao nimeuweka kuweza kuchangia swala hili. Naipongeza Kamati hii kwa kuja na mapendekezo haya. Wengi wa wale amabo wanapata shida sio kwamba hawawezi kufanya kazi, bali kwa sababu mazingira ya kazi sio mazuri kama walivyokuwa wametarajia. Ni bora kwamba kuwe na njia ambayo ikiwa mtu ameshindwa kufanya kazi, kama ni kurejeshe nauli ya ndege, aruhusiwe kurejesha nauli ya ndege na apewe tiketi yake ya ndege kurudi Kenya. Akifika Kenya familia ama wale wahusika warejeshe pesa ya watu ya ndege. Si kwamba mtu aendelee kuzuiliwa, katika sehemu za Ughaibuni bila ya kuwa na nafasi ya kuonana na Wakenya. Tunajua kuwa katika sehemu za kule, sheria yao ni tofauti na sisi. Kule ukipelekwa kama umefanya ajali barabarani, wewe ndio mwenye makosa isipokuwa wewe mwenyewe uweze kuonyesha kwamba hujakuwa na makosa. Njia yao ya sheria ni tofauti na yetu. Hapa nchini unaweza kupelekwa mahakamani ukasema hukufanya, ukapewa bondi ukarudi kufanya kesi yako ukiwa nje. Kwa wale ambao wako katika sehemu kama zile, ni vigumu kuweza kupata nafasi ya kuajiri wakili au kupewa bondi ili utoke huko ukafanye kesi yako ukiwa nje. Hasa ukiwa mgeni bila ya mwenyeji kukusimamia, inakuwa ni vigumu."
}