GET /api/v0.1/hansard/entries/1119539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119539,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119539/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tatizo kubwa pia liko katika Wizara ya Ajira na Huduma za jamii. Ndiyo sababu uwezo wao wa kuwasimamia hawa mawakala ni mdogo sana. Hawawezi kusimamia mawakala wote ambao wanachipuka kila sehemu. Kila sehemu utapata kuna harifu. Ukienda Mombasa sasa hivi utapata kuna mawakala wengi ambao wanafanya kazi hizi. Wengi wanachukua pesa za watu na hawawapeleki kule kazini ambako wameahidi. Vile vile, wengi wameweza kushtakiwa kwa kukosa kulipa pesa za watu ambao wamechukua bila ya kuwapa kazi hizo."
}